MOROGORO.
ZIARA ya waziri mkuu Mizengo Panda wilyani Kilosa imezua jambo baada ya akinamama wa jamii ya wafugaji kuandamana na kulala ofisi nje ya ofisi ya mkuu wa Wilaya hiyo wakitaka kuonana na Waziri Mkuu ili waeleze nia ya serikali dhiidi yao.
Wakizungumza na waandishi nje ya ofisi hiyo juzi (Machi30)majira ya mchana akinamama hao walisema wameamua kuonana uso kwa uso na Pianda ili awatamkie bayana endapo serikali haiwahitaji wafugaji badala ya kuendelea kunyanyasa na kunyang’anywa mifugo kilasiku kwa kigezo cha oparesheni.
Walisema wamechoshwa unyanyasaji huo unaofanywa na serikali kwani umewafanya kishi kama wakimbizi na watuhumiwa wenye kesi kubwakubwa kama za igaidi.
Kwa nyakati tofauti Christina Kyamba,Suma Ndogo na Elizabeth Stelu walikalili kauri ya Mizengo alipokuwa akipokea madaraka aliyonayo bungeni ‘mimi ni mtoto wa mkulima" nakuwa hayo ndio yanyowapa nguvu wakulima na serikali kuwanyanyasa.
Kutokana na vitisho hivyo walisema sasa katika maisha yao na watoto hawana raha kwa kuathirika kisaikolojia jambo ambalo linasababisha kutojishugilisha kabisa na shuguli za maendeleo ikiwemo kwenda shule wakihofia kuuwawa.
Akizungumzia uamuzi wa akina mama hao kutaka kuonana na waziri mkuu Katibu mtendaji wa kitongoji cha Ngaite Islael Kilwaha alisema huo ni uamuzi wa akina mama hao baada ua kuona wanaendelea kupata tabu na watoto huku vitisho kutoka serikalini vikiendelea.
Alisema tukio ha Machi 28 liliendelea kuwatisha akina mama hao na kuwakosesha usingizi na kuwafanya kuendelea kuisha maisha ya wasiwasi kutokana na kisingizio cha oparesheni kinacho fanywa na serikali.
Alisema wafugaji hao sasa wako katika wakti mgumu wa kupatwa magonjwa ya aina mbalimbali ukiwemo Utapiamlo kwa kukosa Nyama na maziwa ambacho ni chakula kikuu cha jamii hiyo.
Hata hivyombali na kushinda kisha kulala ofisini hapo kwa usiku mmoja jana Machi 31 majira ya saa 4,waliteuliwa akina mama wawili akiwemo Christina kyamba na Agnes Kaite kuwasilisha kero zaokwa waziri mkuu ambapo hadi habari inaandikwa hatukupata jibu.
Waziri mkuu Mizengo Pinda yupo mkoani Morogoro hususani katika wilaya ya Kilosa na Mvomero kwa ziara ya siku mbiliambapo anakagua na kupata taarifa mablimbali za maendeleo ya kilimo na tafiti za kilimo.
MOROGORO.
ASKARI wanyama pori kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapa wamefanikiwa kuwakuta wanyama pori kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja akiwafuga bila kibali kibali cha kuruhusiwa kufanya hivyo.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana afisa wanyama pori wilaya ya Morogoro Issa Ndabagenda alisema kuwa askari hao wakiwa katika msako walifanikiwa kuwakuta wanyama aina ya swala mmoja,kobe wanne,komba"bush baby"mmoja wakiwa wanafugwa kwenye banda lililokuwa ndani ya nyumba ya mfanyabiashara mmoja wa mjini hapa aiitwae Malaika.Alisema askari wanaendelea na msako kwa lengo la kukabiliana vitendo hivyo ili kuweza kuwabaini wahusika na kuweza kuwachukulia hatua husika.Hata hivyo alisema walipomhoji mfanyabiashara huyo alidai kuwa wanyama hao aliwaokota wakiwa wadogo na kuwatunza hadi kufikia ukubwa walinao kwa sasa.Alisema mfano kwa swala alimuokota akiwa mdogo na aliweza kumpatia maziwa hadi kuka na kufikia umri alikuwa nao kwa sasa.Afisa wanyama pori huyo alisema msako unaendelea katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Morogoro kwa lengo la kuwabaini watu wanaowafunga wanyama pori bila kuwa na kibali kinachowaruhusu kufanya hivyo.
story by Joseph Malembeka huko kasoro Bahari aka MOROGORO
No comments:
Post a Comment