KOROGWE - TANGA
Wito umetolewa kwa wazazi wote wa Kitanzania kuonyesha ushirikiano na mshikamano katika jukumu la kuwahudumia watoto yatima kwa kuwapenda na kuishi nao bila kuwabagua, kwni hata wao hawakupenda kuishi bila wazazi.
Wito umetolewa kwa wazazi wote wa Kitanzania kuonyesha ushirikiano na mshikamano katika jukumu la kuwahudumia watoto yatima kwa kuwapenda na kuishi nao bila kuwabagua, kwni hata wao hawakupenda kuishi bila wazazi.
Akizungumza na Radio Huruma katibu wanawake Wakatoliki Tanzania Wawata Parokia ya Manundu Korongwe Restiteta Makomba amesema kesho ni siku rasmi ya tukio la Matendo ya huruma kwa Watoto yatima waishio Manundu wilayani Korongwe.
Aidha katibu huyo amesema kusudi la tukio hilo ni kusaidia watoto yatima wenye umri wa miaka 4 hadi 8 kuwasaidia mahitaji mbalimbali, pia kwa kupitia michezo waliyowaandalia watabaini luwa watoto hao wanapata haki zao za msingi au laa.
Bi Makomba amewataka wazazi waondokana na na dhana potofu mara wanapopewa mtoto yatima kumuona kuwa ni mzigo na badala yake wawaone kama baraka, wanahitaji kupendwa, elimu, chakula, malazi na mahitaji mengine muhimu kwani watoto hao wanaishi katika mazingira hatarishi sana kutokana na kukosa wazazi wao.
Akielezea chanzo cha aongezeko la yatima katibu huyo wa Wawata amesema ajali huchangia kwa kiasi kikubwa, ugonjwa wa ukosefu wa kinga mwilini yaani Ukimwi, kuvunjika kwa ndoa pamoja na wazazi kuwabagua watoto wao ndani ya familia zao.
Kauli mbiu katika tukio hilo "Mtoto ni zawadi", pia wazazi wametakiwa kuwaona watoto wote ni sawa, na mtoto wa mwenzako ni wako, hata hivyo hii na mara ya pili ya wana - Wawata kufanya tamasha la matendo ya huruma kwa kutoa misaada mbalimbali kwa yatima waishio Manundu ambapo huduma hiyo hufanyika sambamba na maazimisho ya sherehe ya pasaka kila mwaka, na mwaka huu sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa Mountain View , tarehe 19 mwezi huu kuanzia saa 7 mchana hadi saa kumi jioni.
Story na Zawadi Kika - Korogwe
No comments:
Post a Comment