Imeelezwa kuwa wafadhili wataipa Tanzania takriban dola milioni 470 za kimarekani kwa ajili ya bajeti yake ya mwaka 2009/ 2010.
Kwa mujibu wa Serikali ya Tanzania imesema kwamba benki ya dunia nayo itaipa nchi hiyo dola milioni 220 kuisaidia kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazonufaika kutokana na misaada. Inakabiliwa na athari kubwa kutokana na mgogoro wa kiuchumi ambao umepunguza mahitaji ya bidhaa na bei za bidhaa kama vile kahawa na kupungua kwa watalii wanaoitembelea nchi hiyo.
Ikiwa ni siku tatu tangu benki kuu ya tanzania BOT kutangaza kuwa biashara ya kupanda na kuvuna pesa inayoendeshwa na kampuni DECI Limited ya jijini Dar es aalam katika maeneo mbalimbali hapa nchini ni haramu ,baadhi ya wakazi wa mkoa wa Pwani wamepinga taarifa hiyo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kuwa biashara ya kampuni ya DECI ni halali kwakuwa imesajiliwa kihalali na inaendesha biashara zake kwa kufuata kanuni za mamlaka ya usajili wa makampuni nchini- BRELA.
Mmoja wa wakazi hao Estom Rwegalula, amesema wameshangazwa na taarifa iliyotolewa na benki kuu ya Tanzania BOT kuwa biashara ya kupanda na kuvuna inayofanywa na kampuni ya DECI ni haramu kwani kampuni hiyo imeanza kufanya biashara hiyo ya kupanda na kuvuna kwa zaidi ya miaka mitatu na wakati wote huo imekuwa ikilipa kodi mamlaka ya mapato nchini TRA .
NA ……………………………………
Mke wa rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori, ameilaumu mahakama ya mjini Lima kwa kupitisha hukumu ya kichawi dhidi ya mumewe.
Satomi Kataoka, raia wa Japan mwenye umri wa miaka 42, ameshtushwa na kukasirishwa na hukumu ya miaka 25 iliyotolewa dhidi ya mumewe na jopo la majaji watatu katika mahakama ya mjini Lima nchini Peru baada ya kumpata na hatia kwa makosa ya mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu.

Source:Radio Huruma Fm Habari kwa Ufupi ya saa 8 mchana leo.
Reader:Azalia Lucas Mwimbe
No comments:
Post a Comment