Friday, April 3, 2009

LETS SUPPPORT OUR TEAM!!!!!


HAPA MITAA YA MASIKA MKOANI MOROGORO
Wadau wa soka na michezo kwa ujumla mkoani morogoro wametakiwa kujitoa kikamilifu katika kuisaidia kwa hali na mali timu ya bukinafaso wana kisiki cha mpingo mabingwa wa kandanda mkoa wa morogoro mwaka 2009 ili waweze kujiwinda vizuri na hatua inayofuata.
Wito huo metolewa wadau wa timu hiyo katika hafla ya kuipongeza timu hiyo kwa kuibuka bingwa wa mkoa iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya mwembesongo na kuhudhuriwa na mgeni rasmi diwani wa kata hiyo fransis kayenzi.
Katika hafla hiyo diwani kayenzi ameipongeza timu hiyo kwa kuwa bingwa wa mkoa na kuwataka wadau mbalimbali ndani ndani ya kata hiyo, wilaya na mkoa kila mmoja kwa nafasi yake kuisaidia timu hiyo iweze kufikia malengo yake.
Awali katika risala ya timu hiyo iliyosomwa na katibu mkuu wa timu hiyo nasoro samata imeelezea matatizo na mafanikio ambayo timu imeweza kuyapata kuwa ni pamoja na kushinda michezo 19 kati ya 23 iliyocheza katika ligi hiyo tangu hatua ya wilaya hadi ubingwa wa mkoa na kutoa mfungaji bora mohamed mkingie aliyefunga mabao 8.
Matatizo ambayo timu imeweza kukumbuna nayo ni pamoja na kukimbiwa na wachezaji wake 5 na kocha kwenda timu ya dimon wakati wakiwa katika maandalizi ya ligi hiyo na tatizo la ukata wa fedha jambo ambalo baadaye lilitatuliwa na wafadhili mbalimbali kwa kuichangia timu.
Awali risala hiyo ilibainisha mikakati ya timu hiyo katika kujijenga kiuchumu kuwa ni pamoja na kutaka kuanzisha mradi wa kilimo kununua mashamba ya mpunga na mahindi na kulima mazao yatakayovunwa na kuuzwa kwa manufaa ya klabu hiyo pamoja na mradi wa biashara ya duka.
Hata hivyo pia uongozi wa timu hiyo umewashukuru wadau wote walioisaidia timu katika hali mbalimbali ya kifedha na kimawazo hadi kufikia hapo ilipo na kuwaomba wazidi kuwa nao bega kwa bega katika kipindi hiki wakijiandaa na ligi hiyo ya taifa ngazi ya kanda.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa morogoro aristo niktasi ameipongeza timu hiyo kwa kuibuka bingwa wa mkoa na kusisitiza kuwa hatua inayofuata ni ngumu na inahitaji mshikamano wa pamoja kati ya wachezaji. wadau wa soka, chama cha mpira mkoa na serikali kwa ujumla.
timu hiyo ya bukinafaso yenye wanachama 90 imeanzishwa rasmi mwaka 1985 ikiitwa ‘mafia united’ ikiwa na wanachama 60 kabla ya kubadili jina na kuitwa bukinafaso mwaka 1990 na imewahi kushiriki ligi ya taifa daraja la pili mara kadhaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo mtwara 2002, itigi singida 2003 arusha mwaka 2004, tanga mwaka 2005 na pwani 2006 ilipotolewa na jkt ruvu.

No comments: