UKOSE wa Elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa vijana ni miongoni mwa sababu zinazochangia vijana kujiingiza katika matatizo mbalimbali ikiwemo la mimba za utotoni na maambukizi vvu.Mratibu wa chama cha uzazi na malezi Tanzania(UMATI) mkoani Morogoro Kyarua Robert alisema hayo mijini hapa alipokuwa akizungumza na viongozi mbali mbali wakiwemo wananchi,watu maarufu viongozi wa madhehebu mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs)kutoka wilaya ya Mvomero na manispaa.Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wazazi kuzungumza na watoto wao bila kificho juu ya elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa lengo la kuwasaidia vijana kukua katika maadili mema.Awali wakitoa hoja zao baadhi ya washiriki walisema baadhi ya wazazi husuisani wa kiume kuwaachia jukumu wanawake kulea watoto ni miongoni mwa mambo yanayochangia watoto kujiingiza katika vitendo visivyo vibaya.Ruwely Hamoud alisema tatizo la akina mama kuwashirikisha watoto hasa wa kike katika biashara za uuzaji pombe za kienyeji na mama lishe nyakati za usiku ni miongoni mwa sababu zinazochangia watoto hao kushiriki ngono.Aidha walisema ngoma za asili ni miongoni mwa mambo yanyochangi watoto hususani wa kike kujiingiza kwenye dimbwi la ngono,kupta mambukizi ya vvu na mimba zisizotarajiwa
story by Joseph Malembeka -Morogoro
No comments:
Post a Comment