Friday, July 17, 2009

Picha hii ni Kibaha Picha ya Ndege

JUMLA ya shilingi Bil.500 zimetolewa kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya kusaidia huduma za kijamii nchini Tanzania na watu wa Marekani kupitia ubalozi wake nchini.

Mwakilishi wa ubalozi huo Larry Andre alisema hayo njini hapa wakati akizindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa watoto wenye ulemavu wa akili na kugahrimu zaidi ya Shilingi Mil.7.5

Alisema fedha hizo zilizotolewa mwaka 2009 kusaidia jamii nchini inalengo la kuboresha huduma za kijamii kama kujengea uwezo vyama vya kiraia na masuala ya haki za binadamu kupitia fursa za kiuchumi nakuwa ushirikiano huo utaendelea baina ya nchihizo.

Alifafanua kuwa tayari hivi karibuni shilingi Bil.3.5 zilitolewa kwa ajili ya kuwezesha usalama wa chakula nchini Ghana zitakazo kutumika kukuza tekonolojia ya kisasa kwa wakulima .

Kuhusu mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kituo cha Amani chini ya kanisa katoliki Dayosisi ya Morogoro unalengo la kuboresha lishe na kuongeza pato kituoni hapo
Awali mkurugenzi wa kituo hicho Josephine Bakhita alisema kituo hicho kilichoanzishwa1992 Chamwino mjini Morogoro kimekuwa kutokana na ongezeko la jamii hiyo ambapo matawi mawili yameongezeka likiwemo la Mikese na Mvomero.
Alisema mpaka sasa Amani inajumla ya walemavu zaidi ya 3600 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wilayani Mvomero,kilosa,morogoro vijijini na Manispaa.

Bakhita alisema mradi huo wenye ukubwa wa ekari 11 ambao kituo kilichangia shilingi Mil.3 utapanua kilimo cha awali cha mbogamboga, matunda,mahindi,mpunga na mtama nakuwa utakiwezesha kituo kuongeza pato .

Naye mkuu wa wilaya ya Mvomero Fatuma Mwasa aliwataka wananchi kuthamini michango ya wahisani kwa kuimarisha na kuiendeleza ili kuboresha huduma nyinginezo zikiwemo za afya,elimu,kilimo na Elimu.

Na Joseph Malembeka - Morogoro

No comments: