Wednesday, July 22, 2009

NEWSROOM - RADIO HURUMA


MOROGORO.

BAADHI ya wananchi,Taasisi na Asasi zisizo za kiserikali mkoani Morogoro wamepinga vikali kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo CBF kwamadai kuwa mfuko huo utasababisha mpasuko mkubwa katika jamii na kuhatarisha amani iliyopo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti mjini Morogoro wadau hao walisema mbali na mfuko huo kuwanehemesha wabunge,matumizi ya fedha hizo yatakuwa kinyume na matakwa na kuongeza ufisadi serikalini.

Akizungumzia hoja hiyo Venance Mlali amefafanua kuwa mfuko huo ulionyesha kushindikana katika baadhi ya nchi duniani na barani Afrika utasababisha mgawanyo wa kimasilahi katika Kata na mitaa ndani ya jimbo ikizingatiwa kuwa nchi inamfumo wa vyama vingi

Amesema watu hivi sasa hapa nchini wanaitikadi tofauti za vyama na kuwa hata wabunge wanaochaguliwa huendesha shugli zao kwa misingi na misimamo ya vyama vyao jambo ambalo linweza pia kujitokeza katika matumizi ya fedha hizo.

“Kitakachotokea katika jimbo ni,mbunge wa chama A ataegemea zaidi mitaa ambayo chama chake kimeshika hatam na mitaa yenye wanachama B,C,D,E na F haitafaidi kikamilifu na mfuko”aliongeza Venace.

aidha amesema kwa mujibu wa katiba ya nchi mbunge ni mwakilishi kwenye vikao vya maamuzi bungeni na msimamizi wa shuguli za maendeleo katika jimbo lake nakuwa suala la utekelezaji ni jukumu la serikali kupitia watendaji wake wakiwemo wakurugenzi wa halamashauri na makatibu tawala wa Wilaya na mikoa.

Asheli Kyaruzi na Benadetha Mbaramwezi kwa nyakati toafuti wamesema mbali na mgongano huo pia utaongeza gharama serikalini kwa kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya mfuko huo fedha mabazo zingeingizwa kwenye halmashauri na kufanya kazi nzuri zaidi.

Wamefafanua kuwa bado fedha hizo zitakuwa na mgawanyiko mkubwa ikiwemo kuajili watumishi wapya dhiidi ya mfuko huo badala zingetumika moja kwa moja kwenye kuboreshewa miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii.

Hata hivyo wamehofia ufisadi zaidi katika matumizi ya fedha hizo na kuhoji kuwa endapo matumizi ya fedha katika halmashauri bado ni tete itakuwaje katika mfuko huo ambao hata msimamizi wake si mtaalam wa hesabu badala yake ni mhamasishaji wa maendeleo.

Wamesema bado kunakasoro nyingi ambazo kuwepo kwa mfuko huo Inawezekana kuwaongezea wabunge kiburi cha kuendelea kug’ang’ania katika viti hivyo vya ubunge hadi mwishi wa maisha yao napengine kuwarithisha watoto au wajukuu zao kwa masilahi hayo.



BAGAMOYO
JESHI la polisi mkoa wa Pwani limewatia mbaroni wahamiaji haramu 81 raia wa Somalia wakiwa wamejificha kwenye vichaka vya kijiji cha Masuguru kata ya Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa wakisubiri kusafirishwa na wenyeji wao kwa njia zisizo za halali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Absalom Mwakyoma amesema kuwa walifanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema ambao ni wakazi wa wilaya hiyo.

Mwakyoma amesema kuwa raia hao ambao kati yao 78 ni wanaume na watatu ni wanawake walikutwa wakiwa katika makundi mawili tofauti wakisubiri wenyeji wao kuwatafutia usafiri wa kuwavusha hapa nchini kwenda nchi za jirani ili wasitiwe hatiani kutokana na kukosa vibali.

Aidha Kamanda huyo ameongeza kuwa mbali ya kuwatia mbaroni wahamiaji haramu hao pia waliofanikiwa kukamata magari mawili ambayo yalikuwa kwenye mchakato wa kuwasafirisha wahamiaji hao pamoja na wasindikizaji ambao wanawasaidia raia hao kuvuka hapa nchini kwa kuwapitisha njia za uchochoroni ili wasitiwe mbaroni na vyombo vya dola.

Amewataja waliotiwa mbaroni kuwa ni pamoja na dereva Nurdini Yasini (28)mkazi wa Mabibo jijini Dar es salam,dereva wa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 933 AOR ambalo lilikuwa tayari limepakia wasomalia 30 wakisubiri wenzao waliokuwa wamejificha porini watoke ili waanze safari.

Wengine waliotiwa mbaroni ni pamoja na Mohamed Kibwana (30) mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es salam ambae ni dereva wa gari lenye namba za usajili T 688 AXN Nissan Pick up lililokuwa likisubiri kusafirisha wahamiaji haramu hao.

Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni wasindikizaji wa wahamiaji haramu hao watatu ambao ni pamoja na George Zakaria (35) mkazi wa Msamvu Morogoro, Athumani Hassan (19) mkazi wa Manzese jijini Da es salam pamoja na Hemed Juma(25) mkazi wa jijini Dar es salam.


Hata hivyo Kamanda Mwakyoma amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kutoa taarifa pindi wanapobaini kuwepo kwa wahamiaji haramu katika maeneo yao yao.

WAKATI HUO HUO:SHULE ya shule ya Sekondari ya Luganga iliyopo Wilaya, Mkuranga Mkoani Pwani ipo katika hatari ya kuchomwa moto na kundi la wati wasiofahamika kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutoelewana kati ya mwalimu mkuu wa shule hiyo Ally Kilasama na Diwani wa kata ta Lukanga Sulatan Malenda.

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari lukanga , Alli –kisalama, amemwambia mkuu wa wilaya ya ,mkuranga Henry clemence kuwa tangu uongozi wa shule ulipoteua bodi mpya ya shule na kumuacha diwani wa kata hiyo sultan malenda amekuwa akipigiwa simu yeye pamoja na mwenyekiti wa bodi issa sangiwa kwamba shule hiyo itachomwa moto iwapo ataendelea kuongoza shule hiyo.

Amesema kutokana na tishio hilo yeye pamoja na waalimu wenzake wamekuwa wanaishi katika wasiwasi mkubwa kwani hawajui sababu hasa za kutolewa kwa vitisho hivyo.

Vitisho hivyo vya kuchomwa moto kwa shule ya sekondari lukanga vimekuja wakati diwani sultan malenda akishutumiwa na uongozi wa shule hiyo kwa ubadhirifu wa fedha ujenzi zilizopotea wakati akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule pamoja na tabia yake ya kuingilia mamlaka ya uongozi wa shule .

Hata hivyo diwani, malenda amekanusha vikali tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya mkuranga Sipora Liana amesema ni kweli diwani malenda ana tabia ya kuingilia majukumu na madaraka ya watendaji wa idara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashawishi ili wasusie kufanya shughuli za maendeleo.

Amesema kwamba wamemuaomba mkuu wa kumhakikishia usalama mwalimu ili asihame katika shule hiyo kwani kutasababisha shule hiyo kufa.Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya mkuranga henry clemence amemhskikishia usalama mwalimu mkuu wa shule ya lukenga na kusema kuwa ataimarisha ulinzi katika shule hiyo kwa kuweka askari polisi ambao watakuwa wanalinda shule hiyo usiku na mchana.

Mkuu huyo wa wilaya pia amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo kumpeleka mkaguzi wa ndani kwenda kufanya ukaguzi katika shule hiyo ili kubaini kiasi cha fedha na vifaa vilivyopotea wakati wa ujenzi wa shule hiyo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Tishio la kuchoma moto shule ya sekondari ya lukanga linakuja wakati bado mkoa wa pwani ukiwa bado kwenye jinamizi la uchomaji moto shule za sekondaribaadhi ya wanafunzi kufukuzwa shule huku wengine wakihamishiwa katika shule za sekondari za kata.



No comments: