SERIKALI ya Indonesia mefurahishwa na mazao yanyozalishwa wilayani Muheza mkoani Tanga kwa uzalishaji mazao mbali mbali yakiwemo Matunda,Nafaka na biashara nakuwa ipo haja kuyaboresha ili kukidhi ushindani wa soka la ndani na nje .
Akifunmgua jengo la maonesho ya kilimo katika viwanja vya Mwl.KJ Nyerere-Nanenane mjini Morogoro jana barozi wa nchi hiyo nchini Yudhistiranto Sungadi alisema wilaya hiyo inachangamoto kubwa ya kujitangaza na kutafuta wawekezaji watakao weza kuayaongezea ubora mazao hayo kwa kuyasindika.
Ufunguzi huo pia ulidhudhiliwa na wakuu idara mbalimbali wilayani humo akiwemo Afisa ugavi Wilaya Sefu Shemhina,Afisa kilimo,Mifugo na Ushirika wilaya Dk Isidori Mwezi mpya na mkurugenzi wa Jijijini la Tanga Majuto Mbuguyu.
Aakionyesha kufurahishwa na maandalizi ya maonesho ya wakulima katika banda hilo Barozi Yudhistiranto aliwataka wakulima nchini kutumia maonesho ya aina hiyo katika kanda husika kama ngao ya kufanikisha uboreshaji kilimo na kuondokana na umasikini
Alisema bidhaa nyingi zinazo zalishwa hapa nchini zimekuwa zikikabiliwa na changamo mbalimbali ambazo wakulima wanaweza kuzitatua kupitia maonesho kama hayo nakuwa ili kufanikisha ipo haja kwa serikali kuwawezesha kufika katika maonesho kama hayo ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ya kimaendeleo hususani katika kilimo ambacho ni uti wa mgongo.
Aidha aliwataka waoneshaji kuangalia uwezoakano wa kupunguza gaharama za pembejeo ili wakulima waweze kumudu gaharma hizo na kuzitumia ipasavyo.
Akitoa taarifa ya wilaya hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Eustaki Temu alisema bali na wilaya kubiliwa na ufinyu wa bajeti halamashauri imeweza kutumia shilingi milioni 26 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la hilo la maoenesho katika kipindi cha miaka minne.
Temu alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2005 litatumika kutoa elimu na njia mbali mbali ambazo wamekuwa wakizitumia wakulima na wajasiliamali wadogowado kutoka wilayani humo kwa msimu wa mwaka mzima.
Awali mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bakari Mhando alisema kuwa wakazi wa wilaya ya Muheza ni wakulima,wafugaji na wafanyabiashara ambao wabnahitaji kupata tekenolojia mpya ili kuweza kuoko mazao mengi ambayo yamekuwa yakiharibikia shambani.
Alitaja aina za mazo yanayozalishwa wilayani humo kuwa ni pamoja na kahawa,chai na ufugaji wa ng’ombe na mbuzi wa kisasa katika maeneo ya milimani na mazao ya viungo na mbogamboga,mihogona matunda pamoja yanyopatikana bondeni.
Mwisho
No comments:
Post a Comment