Monday, August 24, 2009

HABARI KWA UFUPI

HABARI KWA UFUPI SAA 8:00 MCHANA.

AUGUST 24.

MADIWANI wa Manispaa ya Arusha, wawacharukia watendaji wa halmashauri hiyo, kwa kutoa hati za kiwanja cha chama cha wakulima na wafugaji

TASO kanda ya kaskazini mara mbili na kuunda tume ili kumbaini aliyehusika na ufisadi huo.

Hayo wameyasema wakati wa kikao cha mwisho cha baraza la madiwanikatika mwaka wa serikali, kilichofanyika ukumbi wa manispaa ya ArushaWamesema kuwa inasikitisha kuona hati inatolewa mara mbili kwa mmiliki mmoja huyo huyo na manispaa ni hiyo hiyo.

SHIRIKA la Afya Duniani WHO limeiteua hospitali teule ya St.Francis wilayani Kilombero mkoani Morogoro kuwa kituo cha ushirikiano na shirika hilo nchini .

Kwa mujibu wa Kaimu mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Anthony Magoda WHO imeiteua hospitali hiyo kuwa kituo chake cha ushirikiano nakuwa ushirikiano utakao husishwa zaidi ni ule wa mafunzo kazini,elimu ya Afya na upasuaji wa dharura.

Dk.Magoda amesema kuwa nafasi hiyo iliyoshindanishwa na hospitali nyingine Nane duniani itaifanya hospitali hiyo kufahamika na kupata mara kwa mara wataalamu wa kimataifa katika tiba za binadamu kupitia mtandao wa shirika hilo WHO.

NA....Serikali ya Yemen imesema wanajeshi wake wamewaua wapiganaji 100 wa kundi la waasi linaloongozwa na kiongozi wa Kishia nchini humo, Abdul Malik al- Houti.

Makamanda wawili wa kundi hilo pia wanasemekana ni miongoni mwa watu waliouawa.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo la waasi amekanusha madai hayo ya serikali.

Tangu mapema Agosti, vikosi vya kijeshi vya Yemen vimekuwa vikipambana vikali na waasi hao , wenye makao yao kaskazini mwa Yemen.

MWISHO WA HABARI KWA UFUPI.

Source Newsroom - Radio Huruma Fm.

No comments: