Friday, August 14, 2009

Am Back

Baada ya wiki kadhaa kutokuwepo sasa am back hususani wewe msikilizaji wangu wa kipindi cha Evening Drive ----- lets share anything going there guys..

by the way nina ishu ya waakulima hapa....


SHIRIKA la mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania MVIWATA limetakiwa kubuni mikakati na mbinu endelevu katika kuboresha huduma za mazao,miundombinu yakiwemo masoko na mfumo kwa wakulima ili kufikia lengo la Kilomo Kwanza.

Katibu mkuu wizara ya kilimo,mifugo na mazingira Zanzibar Khalid Salum Mohamed alisema hayo wakati akifungua mkutano wa kumi na nne wa Mviwata unaokwenda sambamba na warsha ya kitaifa mjini hapa.

Mohamed aliitaka Mviwata kuongeza juhudi za upatikanaji wa taarifa za masoko ili kuwaondolea adha ya masoko ya uhakika wakulima hapa nchini na kuuza mazao yao kwa faida.Mbali na changamoto hiyo katibu huyo pia aliitaka Mviwata kuanzisha mfumo wa takwimu za wanamtandao,ili kupata haraka taarifa za matatizo,mawazo na kutatafutia ufumbuzi haraka kabla hayajathiri uchumi.

Pia alisema mifumo ya kisera imebadilika katika miaka ya nyuma ,sera nyingi zilikuwa zikitungwa bila kushirikisha watu lakini kwa sasa mfumo ambapo ushiriki wa wananchi katika kutunga sera na kutekeleza unasisitizwa na serikali.

"mtandao weni ni jukwaa muhimu sana katika kuhakikisha kwamba mawazo ya wakulima yanazingatiwa katika uandaaji wa sera za kiuchumi na kijamii ambazi zinagusa maslahi ya wakulima,hasa wakulima wadogo"alisema.

Aidha alilitaka shirika hilo kuwa na ziara za mafunzo kwa wakulima kutokana na umuhimu wake wa kubadilishana uzoefu wa mbinu na njia za kutumia kufanikisha uzalishaji9 mkubwa badala ya sasa ambapo kwa kiasi kikubwa hutegemea mipango ya serikali.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa hali ardhi Tanzania Yefred Muyenzi akitoa mada katika warsha hiyo aliishauri serikali kubadilika mfumo wa uwekezaji vijiji kwa kua mara nyingi hutegema maagizo toka serikalikuu badala ya kusubiri mipango ya jamii husika.

Muyenzi alishauri ni vyema kituo cha uwekezaji na serikali kwa ujumla kuhakikisha zinafanya utafiti wa kina juu ya eneo husika na ikiwezekana hata kufika eneo hilo kwa ajili ya kufahamu ukubwa wa eneo linalohitajika kwa ajili ya uwekezaji kama lipo la kutosha na wananchi wanaoishi eneo hilo hawawezi kuathiriwa na uwekezaji huo.

Alisema kumekuwepo na tatizo katika suala zima la utekelezaji wa sheria za ardhi namba nne na tano jambo ambalo linafanya wananchi wakati mwingine ardhi iliyopo katika eneo lao kutolewa kwa mwekezaji.

No comments: