MOROGORO
VIONGOZI wa serikali Mkoa wa Morogoro na wilaya ya Kilosa wamekimbia mkutano wa pamoja uliolenga kuwakutanisha wakulima,wafugaji na waandishi wa habari kwa lengo la kupata ufumbuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.
Mkutano huo uliokuwaumeitishwa na Baraza la habari Tanzania MCT,Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania UTPC na chama cha waandishi wa habari mkoani morogoro MOROPC na kufanyika katika ukumbi wa Savoi pia ulilenga kupokea malalamiko ya wakulima,wafugaji na viongozi wa serikali kuhusiana na oparesheni ya kuwaondoa wafugaji.
Baadhi ya malalamiko ambayo yangepitiwa ni kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa na wilaya Kilosa kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika habari za upande mmoja wa wafugaji kutokana na rushwa inayotolewa na jamii hiyo,huku wafugaji wakilalamikia uongozi wa wilaya na mkoa kutumia kivuli cha operesheni kuwafilisi kwa unyang'anyi wa mifugo katika vijiji vilivyo na usajili halali kisheria .
Pamoja na kupewa barua ya kuudhulia mkutano huo muhimu , mkuu wa mkoa wa Morogoro meja Jenerali mstaafu Said Kalembo na mkuu wa wilaya ya Kilosa ,Athuman Mdoe hawakutokea wala kutuma wawakilishi katika mkutano huo.
Wakizungumza katika mkutano huo wafugaji na wakulima walisikitika kitendo cha viongozi hao Kutohudhulia mkutano huo kwakuwa wao ndio waliokuwa na majibu ya moja kwa moja dhiidi ya madai hayo
Akizungumzia oparesheni ilivyoendeshwa hivi karibuni wilyani kilosa Mkulima Gelvas Mpembwa na Fuime Hanto walisema mbali na zoezi hilo kuhitajika lakini halikuzingatia vigezo vya haki za binadamu ikiwemo kutofahamika kwa idadi ya wahusika katika zopezi hilo na sehemu wanapokwenda.
Wamesema mbali na kutokuwepo kwa vigezo hivyo bado hapakuwa na maandalizi mazuri ya miundombinu kama maji,elimu ya ufugaji na kilimo bora sambamba na ushirikishwaji mbovu wa wafugaji katika vyombo vya maamuzi.
Nao wafugaji Mchungaji Emanuel Ibrahim, Paulo Sawiaati na Ibrahimu Orushoro mbali na kudai kuwa serikali haikuwatendea haki katika utekelezaji zoezi hilo pia walipendekeza kuhakikisha jamii hiyo inapata mwakilishi katika vyombo vya maamuzi likiwemo baraza la madiwani sambamba na serikali kuzitumia vema sheria za ardhi.
Katibu mkuu wa Baraza la Habri Tanzania MCT,Kajubi Mkajanga aliwataka waandishi wa habari Tanzania kutoogopa vitisho vya viongozi na misukosuko inayotolewa na baadhi ya viongozi waandamizi serikalini kwa kuandika matatizo yanyowakabili wananchi kwa bidii zote.
Naye mkurugenzi mtendaji wa UTPC, Abubakar Kassani mbali na kusikitishwa kutotokea kwa viongozi wa serikali katika mkutano huo aliwataka wakulima na wafugaji kushirikiana na waandishi kwa kutoa taarifa za kweli na waandishi kuandika kwa kuzingatia vigezo vya uandishi.
Aidha amewataka waandishi kufichiana siri kwa kukitumia chama chao MOROPC kutatua taflani zao na kuacha tabia mbaya ya kusemana ovyo kwenye ofisi za watu,serikali,taasisi na vilinge kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama na kazi ya mwandishi ambaye ni tegemeo la wanachi hususani walalahoi na jamii kwa jimla.
No comments:
Post a Comment