Friday, March 12, 2010
KUTOKA CHUMBA CHA HABARI - RADIO HURUMA FM
HABARI KWA UFUPI March 12, 2010 SAA 8 MCHANA.
WASAFIRI waliokuwa wakisafiri na basi lenye namba T833ACT mali ya kampuni ya Maburuk wamenusurika kuteketea kwa moto baada ya basi hilo kufuka moshi mbele kwa dereva.
Tukio hilo lililotokea mji mdogo wa Dumila wilayani Kilosa baada ya basi hilo lililokuwa likitokea Dar es sama kuelekea mjini Tabora kuharibika na kuwalaza abilia katika mji huo.Wakisimulia tukio hilo Suzy Patrick na Januari Philopo miongoni mwa abilia hao ambao wamelazimika kuahilisha safari zao na kurudi Morogoro mjini kusubiri usafiri mwingine leo wamesema wameamua kuahilisha wakihofia kulazwa porini hatimae kuporwa mali zao na kupoteza maisha.
HATIMAE serikali imesema utendaji mbovu wa mazoea kwa watumishi wake ndani ya jamii unaifanya kushindwa kufikia malengo ya mipango na mikakati inayo jiwekea badala yake kuifanya kuendelea kutegemea misaada ya nje katika bajeti zake.
Akifungua mkutano wa wachumi wa takwimu na maafisa mipango toka serikali kuu na halamashauri za wilaya nchini Katibu mkuu wa serikali Philemon Luhanjo amesema mbali na rasilimali zilizopo endapo watendaji hawatabadilika na kufanya kazi kwa uhalisia nchi itaendelea kuwa masikini.
NA...Matokeo yanayoendelea kutolewa, kufuatia uchaguzi mkuu nchini Iraq, yanaonesha kuwa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Waziri Mkuu wa zamani, Iyad Alawi, anayewakilisha kundi la vyama visivyokuwa na msimamo wa kidini.
Kundi hilo limelalamika kura kufanyiwa hila ili kumsaidia Waziri Mkuu al-Maliki. Hata hivyo, upande wa waziri mkuu huyo umetupilia mbali shutuma hizo.
MWISHO WA HABARI KWA UFUPI KUTOKA HAPA RADIO HURUMA FM.
Prepared by Evelyn Balozi - News RADIO HURUMA FM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment