Tuesday, April 12, 2011
SEKTA YA KILIMO - TANZANIA
Katika nchi yetu 85% ya Ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo inatumiwa na wakulima wadogo,Sehemu inayobaki inatumiwa na wakulima wakubwa.Wakulima wadogo ni wale wanalima kati ya heka hadi heka 10 hivi na kwa kawaida hutumia nguvu kazi ya wanafamilia wao.Mchango wa sekta ya kilimo kwa mwaka 2003/2004 ilikuwa 48% ya pato la Taifa. Wakulima walichangia kiasi hicho katika pato la Taifa ni wakulima wakubwa na wadogo hasa wale wanaolima mazao ya kibiashara.Wakulima hawa kwa pamoja ni kama 80% ya watanzania wote,lakini miongoni mwao walio wengi ni wakulima wadogo.Hii inasukuma viongozi na wanaotayarisha sera kuelewa jambo hilo ili waweze kutengeneza sera ya kilimo inayojali maslahi na haki za wakulima hasa wakulima wadogo. Ili kuondoa umasikini hatuna budi kuweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo ambayo ndiyo inayobeba watu wengi ambao mi maskini.Lakini mambo ni kinyume kwani sera ya kilimo ya nchi hasa kwa miaka ya hivi karibuni inaonekana inalenga kuwasaidia wakulima wakubwa.Yapo mambo mengi ambayo tumeyaamua wakati yana athari katika sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo. · Uhakika wa Mbegu Kukosekana uhakika wa mbegu huleta tatizo la mazao duni na kukosa uhakika wa chakula na umaskini,Wakulima wamewezoea kuboresha na kuhufadhi mbegu kizazi hadi kizazi. Lakini mwelekeo wa sasa wa kuhimiza mbegu za viini tete ( GMO) utaleta hatari ya kutoweka kwa mbegu za asili kwa sababu mfumo wa kutoa hati miliki kwa mashirika yanayotengeneza mbegu mpya.Lengo linaweza kuwa ni kuua wakulima wetu ili tuwakimbilie watu wa nje.Hivyo kuna kabisa ya kuhamasisha,kuhimiza na pengine kufundisha upya uboreshaji na uhifadhi wa mbegu za asili. · Ujuzi asili wa wakulima ni tatizo lingine kubwa,ujuzi asili unafikiria hapa ni katika maeneo ya mbegu bora,ujuzi katika ukulima na ufugaji ikiwemo matumizi ya dawa za mimea na mifugo pamoja njia asili za kuhifadhi mazao,wagani,walimu,watafiti na serikali wanamuona mkulima kama asiyejua kitu "mjinga" ambaye ni lazima kila wakati aambiwe nini cha kufanya. · Ni kosa kutofungua masikio na kusikiliza kwa makini wakulima wao wanajua mengi na ya kufaa kwa maisha na uhai wa Taifa letu.Tutakapokuwa tayari kuwasikiliza na kuona kazi zao tutaweza kutambua kuwa wakulima wengi wanajua mambo mengi na ya msingi na busara ambayo pengine tunajiona tunajua,lakini hatuyajui,Wakulima wana uwezo wa kujifunza zaidi ikiwa watapewa nafasi na sauti kutoka NGO - Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania - MVIWATA wenye makao makuu mjini Morogoro na wanachama Tanzania nzima bara na visiwani tunaweza kupata mifano mingi ya upeo mkubwa na wakulima wadogo. · SOKO. Katika zama hizi za uchumi wa soko huria wakulima wadogo wameathirika hata kufika hatua ya kukata tamaa haitoshi wala haisaidii kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji ikiwa wanakosa soko la uhakika wa bora.Mambo ni mengi yanayovuna moyo wakulima kwa kukosa soko. Wanunuzi binafsi huwalipa wakulima bei amabyo hailingani kabisa na gharama za uzalishaji.Serikali kuruhusu wafanyabisahra wakubwa kuingiza chakula kutoka nje kwa ushuru na kodi kidogo na kukiuza kwa bei ya chini na wao kupata faida kubwa,Vyakula vinaagizwa wakati mwingine wakulima wetu wa hapa nchini nchini wanavyo nahawana soko hii inaonyesha Serikali kukosa utashi katika kupambana na umaskini kutoruhusu na kutekeleza wakuliam njia ya kuuza mazao yao nje.Mara nyingi tunasikia Serikali ikikemea vikali jambo hilo lakini je kama ni soko huria kwa nini sio haki kwa mkulima mdogo wa mpakani kutumia soko linalomnufaisha zaidi? Kukosekana miundombinu katika maeneo ya uzalishaji Hili ni tatizo lenye sura nyingi na liko wazi kwa wananchi wengi,mkulima wa Sumbawanga,Iringa,Mbeya licha ya kufikisha mazao yake Dar es Salam kuuza kwa bei nzuri ni tatizo kwa sababu ya barabara,Hivyo wakulima hukosa soko na mazao huaribika ama kuuza kwa bei ya kutupa,kwani hata kulifikia soko katika mji mkuu wa wilaya licha ya mkoa ni tatizo kubwa. Kwa sababu ya kukosa nishati viwanda vidogo mfano vya usindikaji na vya kusaga nafaka havipo,maeneo amabyo vingekuwemo na kusaidia mkulima kuuza mazao yake katika bei yenye thamani zaidi ( Value added) kukosa mpango wa hifadhi ya chakula cha dharura inalenga kama soko la ndani na kukuza biashara ya Chakula toka nje,serikali ingeweza kununua chakula kutoka kwa wakulima wetu na kuhifadhi kwa ajiri ya dharura na hapo hapo kumnufaisha mkulima kwa kumpatia soko bora na kumtia moyo kwa kuwa na hakika na soko. Tatizo la soko lingeweza kutatuliwa kwa kila mmoja kuchukua nafasi yake serikali,vikundi vya kijamii na wakulima wenyewe,mfano wakulima kujiunga pamoja kukusanya mazao yao na kuyasafirisha hadi penye soko bora ikiwa na kujipanga vizuri na barabara zitakuwepo. · Mitaji - kuelewa vizuri mitaji ni pamoja na : · mikopo kuwawezeshawakulima kupata pembejeo mazao ( kama soko lipo kuongeza mapato).Imedhihirika mikopo ni tatizo kwa kukosa dhamana inayokubaliwa ama kukopesha chombo kilicho nje ya uwezo wa wakuliam mfano trekta badala ya jembe la kukokotwa na ng'ombe,.kwa kufanya hivi wakulima wakubwa hunufaika zaidi na wale wadogo kuachwa pembeni. · Ardhi; katika hali ya uchumi wa soko huria wapo wawekezaji wa ndani na nje wanaochukua ardhi ya wakulima na kuwakwamisha katika shughuli zao za kilimo. · Imesikika pia kutokea migogoro ya wakulima na wafugaji katika baadhi ya maeneo.Migogoro hii huleta matokeo mabaya na kurudisha nyuma jitihada za wakulima.Serikali ina wajibu wa pekee wa kuzuia migogoro hii. · Ruzuku; Agricultural Sector Development Program ( ASDP ) - Program ya maendeleo ya kilimo inakazia kilimo cha biashara .Nia ni kuwawezesha wakulima wawe wakulima wa bisahra.Ruzuku imeelezwa itatolewa kwa ajili ya viwanda vya usindikaji ( rural agro - business processing Industries ) na kwa wawekezaji binafsi.Pia ruzuku itatolewa kwa ajili ya kukuza nishati endelevu ( jua,upepo na gesi ya samadi ) Hatua hii ingeweza sana lakini hakuna uhakika sana ni kwa vipi ruzuku hiyo itaweza kuwafikia na kuwanufaisha wakulima wadogo.Ikumbukwe kwamba wanasiasa ( wakulima wakubwa ) wanaijua sera kwanza na wanapoona itawanufaisha huanza utekelezaji huku wao wakiwa wameshajiandaa vizuri. Hata hivyo katika ya maandalizi ya ASDP Serikali imeanza kutambua nafasi ya wakulima wadogo na kutafuta njia za kuwapa sauti na nguvu ya ushawishi na utetezi. Huduma za Ugani na mafunzo. Serikali imeamua kukasimu huduma hii kwa sekta binafsi ( NGOs na Mashirika ) kwa njia ya mikataba. Ni vigumu kujua ufanisi wa hatua hii bila kufanya utafiti kujua njia na uwezo uliopo katika miradi na mashirika na pia uwezo wa vikundi na mitandao ya wakulima kuweza kuboresha huduma hii. MAPENDEKEZO. · Katika kumsaidia mkulima mdogo kuondokana na umaskini ni lazima kwanza sote tutambue kuwa umaskini si suala la kiuchumi tu bali ni hasa kukosa uuwezo,nguvu na maadili. · Suala la kilimo sio suala la uzalishaji na pembejeo bali ni suala linalohusu utu wa watu.Kwa hiyo Sera ya kilimo haina budi kujali maslahi na haki za wakulima. · Ni wakulima wenyewe ndiyo wanaweza kujiletea maendeleo na sio serikali wala mashirika fulani.Hivyo mahitaji ya wakulima katika kujiletea maendeleo laazima yawajibike na sera na kuhakikisha utekelezaji wake. · Katika utekelezaji wa Sera ya kilimo unaoendelea hivi sasa,Seriakli itambue nafasi na juhudi za wakulima iwaunge mkono na kuwasaidia katika kujipanga katika vikundi vy amtandao toka vijijini - Taifa Mfano ni muundo wa MVIWATA - kupitia vikundi hivi wakulima washirikishwe katika kutengeneza sera,mipango na mikakati .Serikali itambue na kuheshimu uhuru wa vikundi na mashirika ya wakulima kama vikundi vya kiraia. · Serikali na jamii nzima itambue uwezo wa wakulima na kuwashirikisha katika kusaini mikataba na Serikali hasa Serikali ya wilaya na Sekta binafsi katika kujenga miundombinu kwa ajili ya huduma. · Suala la ruzuku na misaada liangaliwe ili iweze kutolewa mapato ya halmashauri za wilaya.Hii zaidi ingelenga mafunzo katika mambo mbalimbali mfano; kuunda na kuendesha SACCOs. · Serikali hasa katika ngazi ya wilaya na mkoa wajenge mazoea ya kuwafikishia wakulima vijijini taarifa muhimu kwani wakulima katika vikundi vyao wanaweza kuwa daraja kati ya vijiji,kata na wilaya. · Baadhi ya mambo yametengenezwa vizuri,tuache na tabia ya kuzembea utekelezaji. · Elimu juu ya Ukimwi iwafikei watu vijijini kama jitihada zinavyofanyika mijini. Na Frank Odomari - MVIWATA Kwa msaada - Tume ya Haki na Amani "Kwa nini Tunajari."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment