Saturday, July 18, 2009



Miss Morogoro 2009,
sidhani kama mabinti hawa kile ambacho huwa wanaulizwa na majaji wanamaanisha kweli au tu lengo kushiriki tu,lakini pia kwa upande wa zawadi kwa mshindi kwa nii asilipiwe gharama za chuo akaendelea na elimu na si tu kuwapa vitu vya kifahari huku elimu yao inakuwa ni kitendawili kwa jamii!!!ni maoni


Discussion Questions
Hellow! wenzangu wa mawasiliano lets discuss this;

How can a reporter remain independent, unbiased and faithful to the truth if she/he is also to promote peace and reconciliation? Is it possible to be objective in reporting and yet promote humanistic values like peace, unity, and social harmony?


What should be done with extremist language and views in the media, whether it comes from the government or from rebel leaders?’ Is it possible to offer examples of extremist language in the media from the region?

Some scholars have suggested that media freedom implies ‘the freedom to be irresponsible.’ Do you have any reasons to agree or disagree with this view? What are the implications of this view in the volatile context characterized by ethnic, religious, and regional cleavages like the GLR?

Is the news value "media freedom" used to justify peddle false information and rumours that incite violence more important than the need to save human lives? Are there concreate examples of the abuse of media freedom in the region?

Why is the Great Lakes region so prone to conflict? What role can the media play to mitigate conflicts?

Is there any relationship between weak institutions of State (the Police, the Judiciary etc) and the current state of conflict in the region? How do the media in the region undermine institutions of state?

"The Politics of the Belly"(corruption) is said to be a central element in the failure of development in the region. To what extent corruption is a factor in poor media performance in conflict situations?

How can Africa be delivered form ethnic and religious demons that ravage the continent? What is the role of the media in fanning ethnic and other conflicts?

Should the media and journalists involved in hate speech be considered combatants in conflicts? What evidence are in the region’s media showing hate speech etc?

Corruption in the media is sometimes attributed to the failure to reconcile communitarian values (brotherhood, ethnicity etc) and libertarian views like (accuracy, balance etc.)to what extent are the media caught in the communitarian/libertarian dilemma? Viz. Okigbo (1989) suggested the ethnicity is a news value in the Nigerian context whereby news is often analyzed by looking at what ones tribe will lose or gain. Is this true of the Great Lakes region?

Friday, July 17, 2009

Mfanyabishara wa rejareja bidhaa za mbogamboga hapa akichambua njegere tayari kwa kuziuza kwa wateja wake huko mji kasoro bahari Morogoro,Haya ni mazao wakuliwa wetu lakini je huyu mzalishaji anafaidika vipi au bado ananonywa tu kila siku na haoni faida yake?
KAMATI kuu ya ya maandalizi ya maonesho ya nanenane kanda ya mashariki imesema kuwa waziri mkuu Mizengo Pinda Agost 1 anataraji kuwa mgeni rasimi sherehe za maonesho ya wakulima nanenane kanda ya Mashariki mjini Morogoro.

Sherehe hizo zitakazo fungwa na makamu wa rais Dk Ally Mohamed Shein pia zinataraji kuhudhuliwa kwa nyakati tofauti na Mabarozi,Mawaziri na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali yanayoshulika na kilimo Duniani.

Wakati huohuo kamati hiyo iliyokutana juzi katika uwanja wa mwalimu Julius.K.Nyerere imesikitishwa ma maandalizi duni yanayoendelea uwanjani hupo.

Akionyesha kupingana na taarifa kuwa vipando kutomea vizuri inatokana na Moruwasa kutoingiza maji ya kutosha uwanjani humo,Mwenyekiti wa kamati hiyo pia mkuu wa mkoa wa Morogoro Luten kanali mstaafu Issa Machibya alisema kudorola kwa maandalizi hayo kunatokana na uzembe kwa washiriki.

Kamati hiyo ilisema kisingizio cha ukosefu wa maji uwanjani hapo si ya msingi kwakuwa lengo ni kuona vipando kwa tumia njia yoyote kupata maji nasio kutegemea maji toka mamlaka ya majisafi na maji taka Moruwasa.

Wajumbe waliwataka washiriki wa kudumu uwanjani humo ikiwemo TANESCO,Mamlaka ya maji safi na majiraka MORUWASA,waboreshaji barabara,taasisi mashirika na watu mbalimbali kuendelea kuboresha huduma hizo hata baada ya maonesho ili kuufanya uwanja huo kutokuwa tegemezi wakati wa maandalizi.

"Kuhusu maji ipo haja lichimbwe bwawa kubwa litakalo tumika kukinga maji wakati wa mvua za masika na kuyatumia wakati wa kiangazi yanapofanyika maonesho"aliseshauri mjumbe mmoja wapo

Akitoa ufafanuzi wa hali hiyo ya maji Mkurugenzi mtendaji wa malka ya majisafi na majitaka Moruwasa John Mtaita,alikili haliyo kujitokeza nakuwa inatokana na ukame,wizi wa maji katika bomba la uwanjani humo na matumizi yasiyozingatia tatizo hilo.

"naomba kuwa mkweli tu kuhusu tatizo la maji mwaka huu halikwepeki,mamlaka inamaji kidogo sana,na hatahivyo kidogo kinachopatikana kinachepushwa na watu njiani pia matumizi humu uwanjani hayazingatii uhaba unaotukabili"alifafanua Mtaita.

Akitoa ufafanuzi wa changamoto zilizomo uwanjani humo Katibu wa Taso kanda ya mashariki Raphael Jackson alisema Mbali na upungufu wa maji pia Taso inawadai washiriki wake zaidi ya shilingi 86,814,242 zinadaiwa na Taso kanda kutokana na madai mbalimbali.

baadhi ya madeni alitaja kuwa ni pamoja na Mama lishe jumla ya shilingi 930,000,Wizara za serikali Sh.41,141,000,Taasisi zisizo za serikali Sh.4,704,500,Taasisi za serikali Sh.2,567,400, bodi za mazao na mifugo Sh.4,670,000,makampuni Sh.9,423,200,na deni la viwanja na michango Sh.23,378,142.



TAASISI ya Utafiti wa Wanyamapori nchini(TAWIRI) kwa kushirikiana na Mradi wa eneo la Ramser bonde la mto Kilombero(KVRS) wameanzisha mpango wa kusimamia,ukusanyaji na uhifadhi wa taarifa mbalimbali za maliasili 'Kanzudata' zinazopatikana katika bonde la Kilombero.

Wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha madiwani,wafanyakazi wa halmashauri na wafanyakazi wa mradi katika wilaya za Kilombero na Ulanga,Mtafiti Mwandamizi wa wanyamapori kutoka TAWIRI, Honori Maliti walisema chombo hicho kitasaidia kuwa na takwimu sahihi za bonde lianlounganisha wilaya ya Kilombero na Ulanga ulipo mradi wa Ramser.

Maliti alisema mpango huo wa Kanzudata unaotaraji kukabidhiwa mwishoni mwa Agost utasaidia kuwezesha wadau na kuunganisha matumizi ya takwimu sahihi za kitaalamu na zenye ubora unaotakiwa.

Alisema baada ya mpango kukamilika utawezesha mradi na wadau kuweza kufuatilia kwa karibu mabadiliko yanayotokea katika bonde oevu la Kilombero na pia itawezesha kusimamia mradi na kupima matokeo ya hatua kwa kuboresha mazingira ya bonde hilo zikiwemo bionowai.

Awali shauri wa mradi wa Ramser Marcely Madubi alisema mbali na wataalamu na watekelezaji hao kupeata elimu hiyo mpango huo utaanza kusambaza takwimu hizo sehemu mbalimbali hususani wanaohusika na mazingira.

‘Hiyo itakuwa kama kiashiria cha hali halisi ya bonde na kusaidia kufanya maamuzi mbalimbali yanayostahili katika ngazi mbalimbali na ili uhifadhi uendelee na rasilimali ni lazima kutengeneza mpango uishi wa usimamizi wa enao la Ramser la bonde la Kilombero,”alisema.

READY THIS PLZ!!
Faith Satellite Radio and SIGNIS Services Rome Begin a New Phase

Rome, July 1, 2009 ([FSR/SIGNIS) - In June 2007, Faith Satellite Radio™ and SIGNIS collaborated in an effort to reduce the digital divide by providing faith organizations in Africa with a new and innovative way of broadcasting.

Now in 2009, Faith Satellite Radio and SIGNIS Services Rome have entered a new phase to expand services by beginning to offer data and multicasting services to developing countries around the world. FSR's services will no longer be limited to Africa ; but now will be able to include the unreachable parts of the world where a digital solution does not exist.

SIGNIS supports a great number of projects aimed at the development of Radio Broadcasting. For a lot of people in Africa, Latin America and Asia , radio is still the easiest and most direct means of communication available. SIGNIS is collaborating with several international organizations and supplies equipment and training, especially for Africa .

SIGNIS Services Rome (Palazzo San Calisto, Vatican City ) ensures the study and the building of radio stations in Africa . It helps in feasibility financing, buying equipment, training, and instalments of studios, transmitters and aerials.

FSR now offers the proven solution of SSR services that has been exclusive for 50 years. FSR will offer e-learning applications, data solution and/or multi-casting to faith organizations and NGO's around the world so they to can become connected.

Through this next phase, FSR and SSR hope to light up the world with the brightness of computer monitors and fill the air with the sound of the “Good News” for faith and development radio.

For more information, please visit www.faithsatelliteradio.org


SIGNIS, World Catholic Association for Communication
310, rue Royale 1210 Brussels – Belgium
Tel: +32 2 734 97 08 Fax: +32 2 734 70 18
http://www.signis.net
Unsubscribe
Picha hii ni Kibaha Picha ya Ndege

JUMLA ya shilingi Bil.500 zimetolewa kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya kusaidia huduma za kijamii nchini Tanzania na watu wa Marekani kupitia ubalozi wake nchini.

Mwakilishi wa ubalozi huo Larry Andre alisema hayo njini hapa wakati akizindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa watoto wenye ulemavu wa akili na kugahrimu zaidi ya Shilingi Mil.7.5

Alisema fedha hizo zilizotolewa mwaka 2009 kusaidia jamii nchini inalengo la kuboresha huduma za kijamii kama kujengea uwezo vyama vya kiraia na masuala ya haki za binadamu kupitia fursa za kiuchumi nakuwa ushirikiano huo utaendelea baina ya nchihizo.

Alifafanua kuwa tayari hivi karibuni shilingi Bil.3.5 zilitolewa kwa ajili ya kuwezesha usalama wa chakula nchini Ghana zitakazo kutumika kukuza tekonolojia ya kisasa kwa wakulima .

Kuhusu mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kituo cha Amani chini ya kanisa katoliki Dayosisi ya Morogoro unalengo la kuboresha lishe na kuongeza pato kituoni hapo
Awali mkurugenzi wa kituo hicho Josephine Bakhita alisema kituo hicho kilichoanzishwa1992 Chamwino mjini Morogoro kimekuwa kutokana na ongezeko la jamii hiyo ambapo matawi mawili yameongezeka likiwemo la Mikese na Mvomero.
Alisema mpaka sasa Amani inajumla ya walemavu zaidi ya 3600 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wilayani Mvomero,kilosa,morogoro vijijini na Manispaa.

Bakhita alisema mradi huo wenye ukubwa wa ekari 11 ambao kituo kilichangia shilingi Mil.3 utapanua kilimo cha awali cha mbogamboga, matunda,mahindi,mpunga na mtama nakuwa utakiwezesha kituo kuongeza pato .

Naye mkuu wa wilaya ya Mvomero Fatuma Mwasa aliwataka wananchi kuthamini michango ya wahisani kwa kuimarisha na kuiendeleza ili kuboresha huduma nyinginezo zikiwemo za afya,elimu,kilimo na Elimu.

Na Joseph Malembeka - Morogoro




















Evelyn Balozi akiwa katika studio za Radio Huruma Fm (Studio namba 2)hapa akijiandaa kusoma Habari kwa Ufupi,Picha ya juu Azalia Lucas Mwimbe aka Mzee wa Enzi Hizo!!!naye akifanya vitu vyake live on Air..